Friday, February 1, 2019

Hivi Ndivyo Zari Alivyowaumbua Tanasha na Shilole

Hivi Ndivyo Zari Alivyowaumbua Tanasha na Shilole

Mchumba wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch ameendelea kutengeneza vichwa vya habari Bongo, Amani linaye.

Safari hii Tanasha amekuwa gumzo kufuatia gauni alilovaa kwenye pati ya uzinduzi wa pafyumu na taasisi ya Msemaji wa Simba, Haji Sunday Manara, usiku wa kuamkia Jumatatu iliyopita ambalo limeibua mapya.



Gauni hilo la rangi ya bluu linashabihiana kila kitu na lile lililowahi kumuumbua mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ au Shishi Baby miezi kadhaa iliyopita.

Lakini mzazi mwenza wa Diamond, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, yeye alilipatia namna ya kulivaa na kuwaumbua Tanasha na Shilole ambao liliwatia aibu.



TANASHA

Akiwa na Diamond kwenye tukio hilo la Manara lililofanyika katika Ukumbi wa Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel, Posta jijini Dar, Tanasha alikosa kabisa uhuru kufuatia gauni hilo kumvuka na kuacha matiti yake hadharani.



LINAITWA KATA-KIFUA

Gauni hilo maarufu kwa jina la kata-kifua linaloishia kifuani na kuacha mabega wazi lilimfanya Tanasha kushindwa hata kupiga makofi kwani kitendo cha kunyanyua tu mikono na kuachia makwapa, basi lingemvuka lote hadi kiunoni.

Kufuatia hali hiyo, ilibidi Tanasha kulishikilia gauni hilo muda wote huku akimuomba Mungu kimoyomoyo shughuli hiyo imalizike ili aondoke ukumbini hapo kwani alionekana wazi kutokuwa na furaha.



SHILOLE

Miezi kadhaa iliyopita Shilole naye alikuwa gumzo baada ya gauni kama hilo alilokuwa amevaa kwenye pati ya Wasafi Classic Baby (WCB) kumuacha wazi matiti na kumkosesha raha huku akijuta kuvaa nguo hiyo.

Kwenye mitandao ya kijamii, watu walimsimanga mno Shilole kwa kitendo chake cha kuvaa gauni kama hilo na kuacha wazi maungo yake nyeti akiwa ni mwanamke wa Kiislam.


Lakini kama kawaida ya Shilole, siyo mtu wa kuficha mambo, baada ya kuona watu wamemsimanga vya kutosha hakusita kutoa dukuduku lake kuhusu nguo hiyo ambayo iliwaacha watu midomo wazi kwa kumsema.

Shilole alisema kuwa aliliona gauni hilo kwenye mtandao na kuliagiza kwa lengo la kuivaa akiamini kuwa atapendeza na kutokea kama alivyoiona kwenye picha kama ilivyo kawaida ya watu wengi wakiamini kuwa nguo hizo zitawatoa kama walivyoziona katika mtandao.

Shilole alisema: “Yaani kama nitaagiza tena nguo mtandaoni…walahi labda mimi siyo dada Mwajuma.”



ZARI

Baada ya gauni hilo kuwa gumzo, mashabiki wa Zari waliibuka na picha zilizomuonesha mwanamama huyo akiwa amevaa gauni kama hilo na kuwa huru kufanya lolote bila kumvuka.

Picha hizo zilimuonesha Zari akiwa amelivaa gauni kama hilohilo miezi kadhaa iliyopita na kumpendeza bila kujali ni mama wa watoto watano tofauti na Shilole ambaye ni mama wa watoto wawili huku Tanasha akiwa hana mtoto.



MAMA D AMKINGIA KIFUA TANASHA

Wakati mjadala huo ukiwa umenoga huku Tanasha akisemwa kila kona juu ya gauni hilo ndipo alipoibuka ‘mama mkwe’ wake, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ na kumkingia kifua.

Akizungumza na Gazeti la Amani kupitia simu ya kiganjani ya mwanaye Esma Khan, Bi Sandra ambaye ni mama mzazi wa Diamond aliwataka watu wanaomuandama mrembo huyo kuacha kwani wao kama familia wamemkubali alivyo.

“Tanasha ana tabia nzuri na isitoshe ana mapenzi ya dhati kwa familia yetu.



“Anapendwa kushirikiana na familia kwani kuna wakati anaitwa wana familia nyumbani kwake (Mbezi-Beach) na kukaa nao vizuri.

“Kwanza Tanasha hana sifa mbaya na hajawahi kufumaniwa kama wengine,” alisema mama Diamond bila kufafanua aliyefumaniwa ni nani?



ATOA MSIMAMO

Mama huyo aliendelea kufunguka msimamo wa familia kuwa, wanamtambua na kumkubali Tanasha kwani ndiye mwenye vigezo vyote vya kuwa mke wa Diamond.

Kwa upande wake Esma, alisema Tanasha ni zaidi ya wifi kwake kwani anajielewa. Alisema kuhusu mambo mengine yote yanayosemwa kuhusu yeye hawayajali, zaidi wanaangalia tabia zake njema.

DIAMOND NA TANASHA

Diamond na Tanasha wanatarajiwa kutangaza kufunga ndoa muda wowote baada ya kuahirisha zoezi hilo ambalo awali walitangaza lingekuwa ni Februari 14, mwaka huu.

Daimond Awaonya Mbele ya Makonda Wasanii Wanaotoa Rushwa Wasafi Media Ili Ngoma Zao Zichezwe

Daimond Awaonya Mbele ya Makonda Wasanii Wanaotoa Rushwa Wasafi Media I'll Ngoma Zao Zichezwe

Msanii Diamond Platnumz ambae ni bos wa televiesheni ya wasafi ambae pia ni meneja wa ebo ya WCB amefunguka na kuwaonya wasanii ambao wamekuwa wakitoa pesa kwa ajili ya kutaka kupata nafasi za nyimbo zao kupigwa kati atv yake.

Diamond anasema kuwa kwa uande wake alishasema kabisa kuwa kila anaeleta nyimbo yake katika Tv hiyo basi itapigwa lakini kama kuna mtu anakuwa akitaka kutoa pesa ili aweze kupewa muda mwingi wakati kazi yake sio nzuri kuliko wengine basi huyo hana nafasi katika Tv hiyo.



Akiongea katika mkusanyiko mkubwa wa wasanii uliofanyika jana, baada ya mkuu wa mkoa kukutana na wasanii kuzungumzia changamoto za wasanii wa bongo movie , Diamond anasema kuwa tv yake ni bure kabisa na hakuna haja ya kutoa pesa.

Faiza- Nikipata Ukimwi Nitajitangaza Hadharani

Faiza- Nikipata Ukimwi Nitajitangaza Hadharani

Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally amefunguka na kuweka wazi kusababisha endapo siku akijigundua kuwa ni muathirika basi hatajificha bali atajitangaza hadharani.

Faiza amefunguka kuwa endapo itatokea bahati mbaya akakwaa ugonjwa wa Ukimwi a.k.a ngoma, kamwe hatajificha au kujiona tofauti, bali atajitangaza hadharani na kuwapa watu moyo kuwa wanaweza kuishi miaka mingi zaidi.


Katika mahojiano yake na Gazeti la Ijumaa, Faiza ambaye ni mama wa watoto wawili alisema anawashangaa wenye tatizo hilo ambao hujificha na hata wengine kuambukiza wengine, lakini kwa upande wake ataweka hadharani ili kuwapa elimu wengine na kuzuia maambukizi mapya.

Kama mimi ningekuwa na Ukimwi, ningejitangaza hadharani bila woga wowote wala aibu na tena nitasaidia watu wengine wajiepushe na maambuzi mapya“.

Wiki iliyopita Faiza alizua gumzo kwenye Mitandao ya kijamii Baada ya kuposti video iliyomuonyesha akiwa anapima ugonjwa wa Ukimwi na kuanika majibu yake yaliyoonyesha hana maambukizi ya gonjwa hilo.

Wednesday, January 16, 2019

Zijue faida zitokanazo na limau kiafya


Faida za limau au ndimu zinajumuisha matumizi kama tiba kwa ajili ya vidonda vya kooni, matatizo katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya meno, homa, kuvuja damu ndani ya mwili, baridi yabisi, kutibu malengelenge, uzito kupita kiasi, matatizo katika mfumo wa upumuwaji, kipindupindu na shinikizo la juu la damu. Pia ni dawa nzuri kwa ajili ya nywele na ngozi.

Tangu karne nyingi limau linajulikana kama dawa, husaidia pia kuongeza kinga ya mwili, kusafisha tumbo na hujulikana pia kwa kazi yake nzuri ya kusafisha damu.




Juisi ya limau ina faida kadhaa nyingi kama vile kuondoa mchanga katika figo, kupunguza kukamaa kwa mishipa (strokes) na kupunguza joto la mwili. Kama kinywaji ambacho huondoa uchovu mwilini, juisi ya limau itakusaidia kubaki mtulivu na mpole.

Faida nyingi za limau zinatokana na virutubishi vyake vingi mhimu kwa mwili kama vile vitamini C, vitamini B6, vitamini A, vitamini E, folate, niacin thiamin, riboflavin, pantothenic acid, shaba, kalsiamu, chuma, magnesium, potassium, zinki, phosphorus na protini.

Limau ni matunda ambayo yana kitu mhimu sana katika kuondoa sumu mwilini kiitwacho kwa kitaalamu kama “flavonoids” ambacho chenyewe ni mhimu sana katika kupigana na kansa mbalimbali mwilini.

Limau husaidia pia kuzuia matatizo ya kisukari, kufunga choo, shinikizo la juu la damu, homa, husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi vizuri na matatizo mengine mengi yakiwemo kuimarisha ngozi ya mwili, nywele na meno.

Utafiti uliofanywa na Chama cha Madaktari wa magonjwa ya mfumo wa mkojo cha Marekani (American Urological Association) unaonyesha kuwa juisi ya limau au ‘lemonade’ inaweza kuondoa au kuzuia kujitokeza kwa mawe kwenye figo.

Watu hutumia limau na Asali kutengeneza juisi ya limau maarufu kama “lemonade”.

Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau na asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:

*Chukua asali mbichi nusu Lita

*Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata juisi ambayo itakuwa na ujazo wa nusu lita.

Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo.

Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya mdalsini lita 2 ongeza na ya maji ya kawaida lita 1 kupata lita 5. Ihifadhi katika friji isiharibike.

Kunywa robo Lita kutwa mara 2 kwa siku 10 kwa mtu mzima na glasi ndogo moja kwa siku kwa mtoto wa miaka miwili mpaka kumi.

Marashi au harufu ya limau hufukuza mbu, wakati huo huo kuinywa juisi ya limau iliyoongezwa mafuta ya zeituni husaidia kuondoa mchanga katika kibofu cha mkojo. Limau inajulikana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi na hutumika kwa namna nyingi tofauti.

Zifuatazo ni faida mbalimbali za limau mwilini:

1. Kufunga choo na tumbo kushindwa kumeng’enya chakula
Juisi ya limau husaidia kutibu matatizo yahusianayo na tumbo kushindwa kumeng’enya chakula na kufunga choo. Ongeza matone machache ya limau kwenye chakula chako (kuwa makini sababu limau huwa haipatani na maziwa), na itakusaidia katika kumeng’enya chakula.

Limau hufanya kazi kama wakala msafisha damu na mwili kwa ujumla. Na hii ni nzuri kama unapata juisi yako ya limau baada ya chakula cha mchana au cha usiku. Juisi ya limau inatengenezwa kwa kuchanganya maji ya limau, maji kidogo, chumvi ya mawe kidogo na asali au hata sukari. Weka na barafu kidogo pembeni.

Unaweza pia kuongeza majani kidogo ya mnanaa (mint) na mbegu za shamari (fennel seeds) ili kuongezea radha na harufu nzuri. Kunywa juisi hii kila unapokuwa umepata chakula cha mchana cha nguvu au cha jioni.

2. Hutibu homa
Juisi ya limau inaweza kumtibu mtu anayesumbuliwa na homa, mafua au baridi. Limau husaidia kutibu homa kutokana na sifa yake ya kuongeza kiasi cha jasho mwilini.

3. Huongeza afya ya meno
Juisi ya limau mara nyingi imetumika katika kulinda afya ya meno. Kama juisi fresh ya limau itanyunyizwa juu ya jino linalouma inaweza kusaidia kuondoa maumivu. Kusugua (masaji) juisi ya limau juu ya fizi za meno kunaweza kusaidia watu wenye matatizo ya kutokwa damu kwenye fizi huku ikiondoa harufu mbaya katika fizi na mdomo kwa ujumla.

Unaweza kupata faida hizi kama utakuwa unapiga mswaki ukitumia dawa yenye limau ndani yake (lemon tooth paste).

4. Hutunza nywele
Juisi ya limau imejidhihirisha yenyewe kuwa dawa nzuri kwa upande wa matatizo mbalimbali ya nywele. Juisi ya limau ikipakwa kwenye ngozi ya kichwa inaweza kutibu matatizo kama ya mba, kupotea au kukatika kwa nywele, na matatizo mengine yahusuyo nywele na ngozi ya kichwa.

Kama utakuwa ukisafisha nywele zako kwa kutumia juisi au maji ya limau moja kwa moja basi utazifanya nywele zako zipate mng’aro wake wa asili bila gharama yoyote ya ziada.

5. Hulinda ngozi
Kwakuwa Juisi ya limau ni dawa ya asili dhidi ya bakteria, inaweza pia kutibu matatizo mbalimbali ya ngozi. Juisi ya limau inaweza kutumika kupunguza maumivu kwenye ngozi sababu ya kuungua na jua, pia husaidia kupunguza maumivu kutokana na kung’atwa na nyuki. Juisi ya limau au majimaji ya limau yanaweza kutumika kupakaa juu ya ngozi na kutibu chunusi na ukurutu.

Limau pia hutumika kama dawa ya kukufanya usionekane mzee kwakuwa yenyewe huondoa mikunjo na madoadoa ya ngozi.

Kunywa maji ya limau yaliyochanganywa na asali kunasaidia ngozi kuwa na afya zaidi na hata ukipekuwa huko sokoni utazipata baadhi ya sabuni ambazo zimetengenezwa kutokana na limau.

6. Hutibu majeraha ya moto
Upakaji wa maji ya limau (juisi) kwenye eneo la ngozi lililoungua huweza kusaidia makovu kupotea na hii husaidia pia kwa mtu aliyepatwa na malengelenge au vipele vyenye maji maji yanayouma ndani. Na kwa sababu limau ni wakala wa kupooza au wakala mtulizaji (cooling agent), huweza kupunguza maumivu au kuhisi kuungua kwenye ngozi hasa wakati unakuwa na majeraha yanayounguza ngozi.

7. Huzuia kuvujika kwa damu
Limau inayo sifa ya kudhibiti bakteria mwilini (antiseptic properties) na kugandisha damu, sifa hizi au kazi hizi mbili za limau husaidia kusimamisha kuvuja kwa damu ndani ya mwili. Unaweza kutumia maji ya limau ukiweka kwenye kipande cha pamba na kuiweke puani kuzuia pua kuvuja damu.

8. Hupunguza Uzito
Ikiwa utakunywa juisi ya limau iliyochanganywa na asali na maji ya uvuguuvugu, hasa asubuhi tu unapoamka inaweza kusaidia kupunguza uzito.

9. Hutibu matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji
Juisi ya limau husaidia katika kutuliza matatizo katika mfumo wa upumuwaji kama vile pumu. Kwakuwa limau ina kiasi kingi cha vitamini C, husaidia kutibu na kutuliza matatizo ya muda mrefu kwenye mfumo wa upumuwaji.

10. Kipindupindu
Magonjwa kama kipindupindu na malaria yanaweza kutibika kwa kutumia juisi ya limau tu kwa sababu limau hufanya kazi ya kusafisha damu na mwili kwa ujumla.

11. Hutuliza maumivu ya miguu
Limau huwa na harufu ya kuvutia (aromatic) na pia inayo sifa ya kudhibiti bakteria na hutumika kutuliza maumivu au miguu kuwaka moto. Ongeza juisi (maji ya limau) kwenye dishi lenye maji ya moto kidogo na utumbukize miguu kwa dakika kadhaa kwa kuondoa haraka maumivu ya miguu na utajisikia umepata tulizo fulani (relaxed).

12. Baridi Yabisi
Limau au ndimu pia ni kikojoshi, yaani ni kitu kinachosisimua uzalishwaji wa mkojo na kwa sababu hiyo inaweza kutibu baridi yabisi na maumivu ya kwenye mishipa. Husaidia kutoa nje bakteria wabaya na sumu mbalimbali mwilini.

13. Hutibu malengelenge (Corns)
Juisi ya limau inaweza kusaidia kukausha malengelenge au vipele ambavyo huwa na majimaji ambavyo hujitokeza mara nyingi chini ya unyayo au katikati ya vidole vya mikono. Kunywa juisi ya limau na maji ndani yake husaidia wagonjwa kupunguza mawe kwenye nyongo.

14. Hutibu maambukizi ya kwenye koo
Limau ni tunda bora kabisa ambalo hupigana dhidi ya matatizo yanayohusiana na maambukizi kooni sababu ya sifa yake kubwa ya kudhibiti bakteria mwilini.

15. Hutibu shinikizo la juu la damu
Kunywa juisi ya limau kuna msaada mkubwa kwa watu wenye matatizo ya moyo kwa sababu limau lina kiasi cha kutosha cha potasiamu. Limau hudhibiti shinikizo la juu la damu, kizunguzungu, na uchovu sugu kwa sababu yenyewe limau hutoa hisia za utulivu kwa mwili na roho pia. Mara nyingi limau imetumika kwa watu wenye mfadhaiko wa akili na majonzi.

Dalili nne ambazo ukiziona kwenye mahusiano ujue mnaendana



Wataalamu wa mahusiano wanasema kuwa kuna dalili nne ambazo ukiziona kwenye mahusiano yako basi amini kuwa ninyi mnaendana na pia mapenzi yenu yatadumu

1. Uhusiano wenu uwe na uwiano.

Mahusiano ambayo yamefanikiwa ni yale yenye uwiano sahihi. Katika mahusiano mtakuwa tofauti wakati mwingine, na utofauti huu lazima ulete ulingano.

Mfano, kuna ambao hupenda sana kutoka out na marafiki, huyu anahitaji kupata mtu ambaye si mpenzi sana wa kwenda out ili kuleta mlingano. Unatakiwa kuwa na mtu ambaye unakamilika unapokuwa nae, mtu ambaye mkiwa pamoja mkichanganya tabia zenu mnapata tabia moja ambayo imetokana na kuathiriana kwa matendo yenu.

2. Mnafurahia kusafiri pamoja.

Njia rahisi kabisa ya kujua kama mnaendeana ni kama manafurahia mnapokuwa manasafiri pamoja, Watu wanaoendana hupenda kusafiri pamoja na kwenda sehemu tofauti tofauti.

 Kama wewe unataka kusafiri kwa gari, lakini mwenzako anataka kupanda ndege na ubishani wenu unakuwa mkubwa basi ujue ninyi manatatizo. Wapenzi wanaoendana hukubaliana na njia moja ya kutumia ambayo wote wataifurahia.

3. Uliyenaye anakufanya ujisikie vizuri.

Kuwa katika mahusiano ambayo yanakufa ujisikie kuwa upo katika ubora wako, sio mahusiano ambayo kila ukiyakumbuka unanuna.Kuwa na uhusiano na mtu ambaye mkikaa pamoja huhitaji kupiga miayo na kujinyoosha ili upate cha kuongea. Kuwa na mahusiano ambayo yanakufanya uone fahara hata kuyazungumzia mbele ya rafiki zako.

4. Kuna kitu mnachokipenda ambacho mnafurahia kukifanya pamoja.

Hii ni muhimu kuiona, watu wanaopendana huwa kuna kitu kimoja au zaidi ambavyo wote mnapenda na hufurahia kukifanya pamoja. Hii haimaanishi kuwa basi vitu vyenu kama ni muziki, au vitu vingine vitakuwa sawa, lakini kuna kitu ambacho kitakuwa kinaingiliana kati yenu na ambacho mnafurahia kukifanya.

Kwa ufupi mtakuwa na labda vitu viwili au vitatu mnavyopenda kufanya pamoja mfano kuogelea, kuangalia tamthiliya, muziki, kutembea na vingine. Hii ni ishara kuwa ninyi

Ni kweli mapenzi yana maumivu makali lakini unaweza kuyasahau




Ni wiki nyingine mpenzi msomaji wa safu hii tunakutana tena jamvini hapa kwa neema na rehema za Mwenyezi Mungu. Leo tunaangalia ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kuwa sumu kali inayosambaa kwa haraka sana katika miili ya wanadamu wa jinsia zote.

Ni kweli kwamba, mapenzi yanatesa kuliko kitu chochote katika uso wa dunia hii. Ni mapenzi hayohayo ambayo yana nguvu na maumivu makali kuliko maumivu ya kitu chochote unachokijua chenye kusababisha maumivu.

Pia ni kweli wapo watu wengi wameumizwa na kuteswa na mapenzi. Wengine wanaendelea kuteseka na kuumia kila siku. Wengine wanatamani kuyaepuka ingawa hawawezi zaidi ya kupumzika kwa muda. Wapo wanaotamani kuyakimbia ila hayakimbiliki. Wengine wanatamani kujiua ila roho wa Mungu anawashindia.

Inawezekana ni kweli mpenzi wako amekuumiza sana lakini vumilia kwani maumivu hayo ni ya muda na ninaamini ipo siku utayasahau.

Maumivu unayoyapata kwa sababu ya mke, mpenzi, mchumba au mume wako ni ya mpito tu, ni kama masika na kiangazi kinavyoikumba ardhi, mara nyingi huwa ni kwa mpito.

Kuna msemo ambao hutumika sana katika dunia tuliyonayo usemao ‘hakuna marefu yasiyokuwa na ncha’. Hakika maneno haya yana ukweli f’lani ndani yake na ndivyo ilivyo kwamba, mapenzi yanaumiza, yanatesa, yanasumbua ila maumivu yake yana mwisho. Haijalishi umeumia, umeteswa kwa muda au namna gani lakini amini siku yaja nawe utapona na kurudi katika hali yako ya zamani.

Usimchukie aliyekuumiza na kukutesa katika mapenzi, amini ni sehemu ya maisha yako, ulipaswa kuyapita.

Wapenzi wengi wamekuwa wakiteseka mno na namna ya kuwasahau wenza wao baada ya kutengena au kuachwa. Baada ya mada ya wiki iliyopita nilipokea simu ya msomaji wangu kutoka jijini Mwanza akilalamika kuwa ameachana na mpenzi wake aliyedumu naye kwa miaka minne lakini kinachomtesa akilini mwake ni fikra na mapenzi juu ya mpenzi wake huyo.

KIMSINGI IKO HIVI;
Kwa sababu ya mazoea na kushirikiana katika masuala au vitu vingi na mpenzi wako ndiyo maana huwa ni vigumu sana kumsahau lakini baada ya muda naamini unaweza kusahau. Kipindi cha maumivu ya mapenzi ni kama kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu ambapo kila mtu anatamani chama chake kishinde na kama kipindi hiki cha uchaguzi kikitumika vibaya na kusababisha uvunjifu wa amani, basi wananchi wa nchi husika watakuwa wamekosa busara kwani uchaguzi ni suala la mpito na ndivyo ilivyo kwa maumivu ya mapenzi, huwa ni suala la mpito tu.

Sababu za wanaume kuwa mapenzini na wafanyakazi wa ndani (house girls)



Miongoni mwa watu ambao wanatakiwa kupewa heshima zote hapa duniani ni wadada wa kazi za nyumbani ( house girl),  maana hawa wamekuwa wana msaada mkubwa sana katika familia zilizo nyingi. Wamekuwa wakiwasaidia wenye nyumba katika kutimiza majumu mbalimbali ambapo mimi binafsi naamini kazi hizo wanazozifanya na wafanyakazi hao  kama wenye nyumba wakipewa wazifanye ni lazima zitawashinda hii ni kutokana na ugumu na wingi wa kazi hizo.

Lengo la kuja hapa si kuwasifia wadada wa kazi ila nafanya hivyo kwa sababu najikuta naguswa sana na umuhimu wa wadada wa kazi katika kutekeleza majukumu mbalimbali wayafanyayo. Kama wewe ni mdada wa kazi na unasoma makala hii basi mwenyezi Mungu akautie nguvu kila wakati katika kutekeleza  yaliyo mema na yenye kumpendaza bosi wako.

Baada ya kusema hayo naomba sasa naomba nilonge na wakina mama wote walioko kwenye mahusiano ya  ndoa ambao wanaishi na wafanyakazi wa ndani.

Hivi uliwahi kujiuliza ni kwanini wanaume wengi hupenda kuwa na mahusiano na wasichana wa ndani? Kama hujawahi kujiuliza basi leo nitakupa ukweli usiojua kuhusu jambo hili.

Ipi hivi wanandoa wanapoingia katika mahusiano ya kimapenzi huwa kunakuwepo na upendo wa kweli baina yao mwanzoni kabisa mwa mahusiano hayo ila kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo upendo unavyozidi kushuka, jambo hili hutokea hii ni kwa sababu ya wanandoa hao hufika hatua wanazoeana sana hivyo kila mmoja wao kumuona mwenzake ni mtu wa kawaida sana hivyo kupelea kushuka kwa heshima baina yao.

Hivyo inapofika hatua ya kwamba wandoa hao wamezoea na heshima imeshuka hivyo ndoa hubadilika mwelekeo na kuwa chungu kama shubiri,  na inapofika hatua hii mwanaume huwa haoni thamani tena ya mkewe.

Na kwa kuwa falsafa ya mahusiano inatuambia ya kwamba mwanaume huwa haitaji upendo kutoka kwa mkewe  katika suala zima zima la mahusiano, bali mwanaume huhitaji heshima ya kutosha kutoka kwa mke wake, hivyo inapofika kipindi mwanaume huyo haoni tena thamani na upendo kutoka kwa mkewe hivyo anaamua kung`aza macho yake kwa mtu ambaye atampa heshima.

Na kwa kuwa wewe mkewe umebadilika kitabia haupo kama ulivyokuwa zamani hivyo mwanaume huyo anaamua kwenda kwa mfanyakazi wako wa ndani, kwa kuwa mwanaume anaona heshima nyingi kutoka kwa mfanyakazi wa ndani kuliko kwako.

Nini kifanyike ili kuzua tabia ya mwanaume kutoka kimapenzi na wafanyakazi wa ndani.

Mosi; ewe mwanamke  ili mwanaume wako  asiwe na tabia hii ya kuwapenda kimapenzi wafanyakazi wako wa ndani unatakiwa kuelewa ya kwamba kitu ambacho humpa mwanaume tabasamu mwanana la kimapenzi ni pamoja na kumuonesha mwanaume huyo heshima iliyo ya kweli na si vinginevyo.

Pia si kila jukumu anatakiwa kufanya mfanyakazi wako wa ndani mengine unatakiwa kufanya wewe mwenyewe, kila wakati kumbuka majukumu yako ni yapi na majukumu ya kumpa mfanyakazzi wako ni yapi pia.

Mbili; Mwanaume achana na tabia hii kwani haitakusaidia kwa chochote zaidi ya kujenga mahusiano yaliyo mabovu baina yako na mpenzi wako. Lakini pia Afisa Mipango nakushauri ya kuwa kila wakati ewe mwanaume unatakiwa kukumbuka kiapo chako cha ndoa.

Tatu; Ewe mfanyakazi wa ndani tafadhari sana achana mara moja na tabia hiyo ya kufanya unayajua sana mapenzi, kilichokupelekea hapo ni kufanya kazi na si mengineyo kwani kama utaendelea na tabia hiyo utaweka sumu kwenye familia hiyo.  Muombe Mungu akupe na nawe kipenzi wa moyo wako.

Mwisho naomba nikutakie siku njema na majumu mema, endelea kutembelea Muungwana blog kila wakati.

Na. Benson Chonya

Hivi Ndivyo Zari Alivyowaumbua Tanasha na Shilole

Mchumba wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch ameendelea kutengeneza vichwa vya habari Bongo, Amani linaye....