Wednesday, January 16, 2019

Zijue faida zitokanazo na limau kiafya


Faida za limau au ndimu zinajumuisha matumizi kama tiba kwa ajili ya vidonda vya kooni, matatizo katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya meno, homa, kuvuja damu ndani ya mwili, baridi yabisi, kutibu malengelenge, uzito kupita kiasi, matatizo katika mfumo wa upumuwaji, kipindupindu na shinikizo la juu la damu. Pia ni dawa nzuri kwa ajili ya nywele na ngozi.

Tangu karne nyingi limau linajulikana kama dawa, husaidia pia kuongeza kinga ya mwili, kusafisha tumbo na hujulikana pia kwa kazi yake nzuri ya kusafisha damu.




Juisi ya limau ina faida kadhaa nyingi kama vile kuondoa mchanga katika figo, kupunguza kukamaa kwa mishipa (strokes) na kupunguza joto la mwili. Kama kinywaji ambacho huondoa uchovu mwilini, juisi ya limau itakusaidia kubaki mtulivu na mpole.

Faida nyingi za limau zinatokana na virutubishi vyake vingi mhimu kwa mwili kama vile vitamini C, vitamini B6, vitamini A, vitamini E, folate, niacin thiamin, riboflavin, pantothenic acid, shaba, kalsiamu, chuma, magnesium, potassium, zinki, phosphorus na protini.

Limau ni matunda ambayo yana kitu mhimu sana katika kuondoa sumu mwilini kiitwacho kwa kitaalamu kama “flavonoids” ambacho chenyewe ni mhimu sana katika kupigana na kansa mbalimbali mwilini.

Limau husaidia pia kuzuia matatizo ya kisukari, kufunga choo, shinikizo la juu la damu, homa, husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi vizuri na matatizo mengine mengi yakiwemo kuimarisha ngozi ya mwili, nywele na meno.

Utafiti uliofanywa na Chama cha Madaktari wa magonjwa ya mfumo wa mkojo cha Marekani (American Urological Association) unaonyesha kuwa juisi ya limau au ‘lemonade’ inaweza kuondoa au kuzuia kujitokeza kwa mawe kwenye figo.

Watu hutumia limau na Asali kutengeneza juisi ya limau maarufu kama “lemonade”.

Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau na asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:

*Chukua asali mbichi nusu Lita

*Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata juisi ambayo itakuwa na ujazo wa nusu lita.

Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo.

Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya mdalsini lita 2 ongeza na ya maji ya kawaida lita 1 kupata lita 5. Ihifadhi katika friji isiharibike.

Kunywa robo Lita kutwa mara 2 kwa siku 10 kwa mtu mzima na glasi ndogo moja kwa siku kwa mtoto wa miaka miwili mpaka kumi.

Marashi au harufu ya limau hufukuza mbu, wakati huo huo kuinywa juisi ya limau iliyoongezwa mafuta ya zeituni husaidia kuondoa mchanga katika kibofu cha mkojo. Limau inajulikana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi na hutumika kwa namna nyingi tofauti.

Zifuatazo ni faida mbalimbali za limau mwilini:

1. Kufunga choo na tumbo kushindwa kumeng’enya chakula
Juisi ya limau husaidia kutibu matatizo yahusianayo na tumbo kushindwa kumeng’enya chakula na kufunga choo. Ongeza matone machache ya limau kwenye chakula chako (kuwa makini sababu limau huwa haipatani na maziwa), na itakusaidia katika kumeng’enya chakula.

Limau hufanya kazi kama wakala msafisha damu na mwili kwa ujumla. Na hii ni nzuri kama unapata juisi yako ya limau baada ya chakula cha mchana au cha usiku. Juisi ya limau inatengenezwa kwa kuchanganya maji ya limau, maji kidogo, chumvi ya mawe kidogo na asali au hata sukari. Weka na barafu kidogo pembeni.

Unaweza pia kuongeza majani kidogo ya mnanaa (mint) na mbegu za shamari (fennel seeds) ili kuongezea radha na harufu nzuri. Kunywa juisi hii kila unapokuwa umepata chakula cha mchana cha nguvu au cha jioni.

2. Hutibu homa
Juisi ya limau inaweza kumtibu mtu anayesumbuliwa na homa, mafua au baridi. Limau husaidia kutibu homa kutokana na sifa yake ya kuongeza kiasi cha jasho mwilini.

3. Huongeza afya ya meno
Juisi ya limau mara nyingi imetumika katika kulinda afya ya meno. Kama juisi fresh ya limau itanyunyizwa juu ya jino linalouma inaweza kusaidia kuondoa maumivu. Kusugua (masaji) juisi ya limau juu ya fizi za meno kunaweza kusaidia watu wenye matatizo ya kutokwa damu kwenye fizi huku ikiondoa harufu mbaya katika fizi na mdomo kwa ujumla.

Unaweza kupata faida hizi kama utakuwa unapiga mswaki ukitumia dawa yenye limau ndani yake (lemon tooth paste).

4. Hutunza nywele
Juisi ya limau imejidhihirisha yenyewe kuwa dawa nzuri kwa upande wa matatizo mbalimbali ya nywele. Juisi ya limau ikipakwa kwenye ngozi ya kichwa inaweza kutibu matatizo kama ya mba, kupotea au kukatika kwa nywele, na matatizo mengine yahusuyo nywele na ngozi ya kichwa.

Kama utakuwa ukisafisha nywele zako kwa kutumia juisi au maji ya limau moja kwa moja basi utazifanya nywele zako zipate mng’aro wake wa asili bila gharama yoyote ya ziada.

5. Hulinda ngozi
Kwakuwa Juisi ya limau ni dawa ya asili dhidi ya bakteria, inaweza pia kutibu matatizo mbalimbali ya ngozi. Juisi ya limau inaweza kutumika kupunguza maumivu kwenye ngozi sababu ya kuungua na jua, pia husaidia kupunguza maumivu kutokana na kung’atwa na nyuki. Juisi ya limau au majimaji ya limau yanaweza kutumika kupakaa juu ya ngozi na kutibu chunusi na ukurutu.

Limau pia hutumika kama dawa ya kukufanya usionekane mzee kwakuwa yenyewe huondoa mikunjo na madoadoa ya ngozi.

Kunywa maji ya limau yaliyochanganywa na asali kunasaidia ngozi kuwa na afya zaidi na hata ukipekuwa huko sokoni utazipata baadhi ya sabuni ambazo zimetengenezwa kutokana na limau.

6. Hutibu majeraha ya moto
Upakaji wa maji ya limau (juisi) kwenye eneo la ngozi lililoungua huweza kusaidia makovu kupotea na hii husaidia pia kwa mtu aliyepatwa na malengelenge au vipele vyenye maji maji yanayouma ndani. Na kwa sababu limau ni wakala wa kupooza au wakala mtulizaji (cooling agent), huweza kupunguza maumivu au kuhisi kuungua kwenye ngozi hasa wakati unakuwa na majeraha yanayounguza ngozi.

7. Huzuia kuvujika kwa damu
Limau inayo sifa ya kudhibiti bakteria mwilini (antiseptic properties) na kugandisha damu, sifa hizi au kazi hizi mbili za limau husaidia kusimamisha kuvuja kwa damu ndani ya mwili. Unaweza kutumia maji ya limau ukiweka kwenye kipande cha pamba na kuiweke puani kuzuia pua kuvuja damu.

8. Hupunguza Uzito
Ikiwa utakunywa juisi ya limau iliyochanganywa na asali na maji ya uvuguuvugu, hasa asubuhi tu unapoamka inaweza kusaidia kupunguza uzito.

9. Hutibu matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji
Juisi ya limau husaidia katika kutuliza matatizo katika mfumo wa upumuwaji kama vile pumu. Kwakuwa limau ina kiasi kingi cha vitamini C, husaidia kutibu na kutuliza matatizo ya muda mrefu kwenye mfumo wa upumuwaji.

10. Kipindupindu
Magonjwa kama kipindupindu na malaria yanaweza kutibika kwa kutumia juisi ya limau tu kwa sababu limau hufanya kazi ya kusafisha damu na mwili kwa ujumla.

11. Hutuliza maumivu ya miguu
Limau huwa na harufu ya kuvutia (aromatic) na pia inayo sifa ya kudhibiti bakteria na hutumika kutuliza maumivu au miguu kuwaka moto. Ongeza juisi (maji ya limau) kwenye dishi lenye maji ya moto kidogo na utumbukize miguu kwa dakika kadhaa kwa kuondoa haraka maumivu ya miguu na utajisikia umepata tulizo fulani (relaxed).

12. Baridi Yabisi
Limau au ndimu pia ni kikojoshi, yaani ni kitu kinachosisimua uzalishwaji wa mkojo na kwa sababu hiyo inaweza kutibu baridi yabisi na maumivu ya kwenye mishipa. Husaidia kutoa nje bakteria wabaya na sumu mbalimbali mwilini.

13. Hutibu malengelenge (Corns)
Juisi ya limau inaweza kusaidia kukausha malengelenge au vipele ambavyo huwa na majimaji ambavyo hujitokeza mara nyingi chini ya unyayo au katikati ya vidole vya mikono. Kunywa juisi ya limau na maji ndani yake husaidia wagonjwa kupunguza mawe kwenye nyongo.

14. Hutibu maambukizi ya kwenye koo
Limau ni tunda bora kabisa ambalo hupigana dhidi ya matatizo yanayohusiana na maambukizi kooni sababu ya sifa yake kubwa ya kudhibiti bakteria mwilini.

15. Hutibu shinikizo la juu la damu
Kunywa juisi ya limau kuna msaada mkubwa kwa watu wenye matatizo ya moyo kwa sababu limau lina kiasi cha kutosha cha potasiamu. Limau hudhibiti shinikizo la juu la damu, kizunguzungu, na uchovu sugu kwa sababu yenyewe limau hutoa hisia za utulivu kwa mwili na roho pia. Mara nyingi limau imetumika kwa watu wenye mfadhaiko wa akili na majonzi.

Dalili nne ambazo ukiziona kwenye mahusiano ujue mnaendana



Wataalamu wa mahusiano wanasema kuwa kuna dalili nne ambazo ukiziona kwenye mahusiano yako basi amini kuwa ninyi mnaendana na pia mapenzi yenu yatadumu

1. Uhusiano wenu uwe na uwiano.

Mahusiano ambayo yamefanikiwa ni yale yenye uwiano sahihi. Katika mahusiano mtakuwa tofauti wakati mwingine, na utofauti huu lazima ulete ulingano.

Mfano, kuna ambao hupenda sana kutoka out na marafiki, huyu anahitaji kupata mtu ambaye si mpenzi sana wa kwenda out ili kuleta mlingano. Unatakiwa kuwa na mtu ambaye unakamilika unapokuwa nae, mtu ambaye mkiwa pamoja mkichanganya tabia zenu mnapata tabia moja ambayo imetokana na kuathiriana kwa matendo yenu.

2. Mnafurahia kusafiri pamoja.

Njia rahisi kabisa ya kujua kama mnaendeana ni kama manafurahia mnapokuwa manasafiri pamoja, Watu wanaoendana hupenda kusafiri pamoja na kwenda sehemu tofauti tofauti.

 Kama wewe unataka kusafiri kwa gari, lakini mwenzako anataka kupanda ndege na ubishani wenu unakuwa mkubwa basi ujue ninyi manatatizo. Wapenzi wanaoendana hukubaliana na njia moja ya kutumia ambayo wote wataifurahia.

3. Uliyenaye anakufanya ujisikie vizuri.

Kuwa katika mahusiano ambayo yanakufa ujisikie kuwa upo katika ubora wako, sio mahusiano ambayo kila ukiyakumbuka unanuna.Kuwa na uhusiano na mtu ambaye mkikaa pamoja huhitaji kupiga miayo na kujinyoosha ili upate cha kuongea. Kuwa na mahusiano ambayo yanakufanya uone fahara hata kuyazungumzia mbele ya rafiki zako.

4. Kuna kitu mnachokipenda ambacho mnafurahia kukifanya pamoja.

Hii ni muhimu kuiona, watu wanaopendana huwa kuna kitu kimoja au zaidi ambavyo wote mnapenda na hufurahia kukifanya pamoja. Hii haimaanishi kuwa basi vitu vyenu kama ni muziki, au vitu vingine vitakuwa sawa, lakini kuna kitu ambacho kitakuwa kinaingiliana kati yenu na ambacho mnafurahia kukifanya.

Kwa ufupi mtakuwa na labda vitu viwili au vitatu mnavyopenda kufanya pamoja mfano kuogelea, kuangalia tamthiliya, muziki, kutembea na vingine. Hii ni ishara kuwa ninyi

Ni kweli mapenzi yana maumivu makali lakini unaweza kuyasahau




Ni wiki nyingine mpenzi msomaji wa safu hii tunakutana tena jamvini hapa kwa neema na rehema za Mwenyezi Mungu. Leo tunaangalia ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kuwa sumu kali inayosambaa kwa haraka sana katika miili ya wanadamu wa jinsia zote.

Ni kweli kwamba, mapenzi yanatesa kuliko kitu chochote katika uso wa dunia hii. Ni mapenzi hayohayo ambayo yana nguvu na maumivu makali kuliko maumivu ya kitu chochote unachokijua chenye kusababisha maumivu.

Pia ni kweli wapo watu wengi wameumizwa na kuteswa na mapenzi. Wengine wanaendelea kuteseka na kuumia kila siku. Wengine wanatamani kuyaepuka ingawa hawawezi zaidi ya kupumzika kwa muda. Wapo wanaotamani kuyakimbia ila hayakimbiliki. Wengine wanatamani kujiua ila roho wa Mungu anawashindia.

Inawezekana ni kweli mpenzi wako amekuumiza sana lakini vumilia kwani maumivu hayo ni ya muda na ninaamini ipo siku utayasahau.

Maumivu unayoyapata kwa sababu ya mke, mpenzi, mchumba au mume wako ni ya mpito tu, ni kama masika na kiangazi kinavyoikumba ardhi, mara nyingi huwa ni kwa mpito.

Kuna msemo ambao hutumika sana katika dunia tuliyonayo usemao ‘hakuna marefu yasiyokuwa na ncha’. Hakika maneno haya yana ukweli f’lani ndani yake na ndivyo ilivyo kwamba, mapenzi yanaumiza, yanatesa, yanasumbua ila maumivu yake yana mwisho. Haijalishi umeumia, umeteswa kwa muda au namna gani lakini amini siku yaja nawe utapona na kurudi katika hali yako ya zamani.

Usimchukie aliyekuumiza na kukutesa katika mapenzi, amini ni sehemu ya maisha yako, ulipaswa kuyapita.

Wapenzi wengi wamekuwa wakiteseka mno na namna ya kuwasahau wenza wao baada ya kutengena au kuachwa. Baada ya mada ya wiki iliyopita nilipokea simu ya msomaji wangu kutoka jijini Mwanza akilalamika kuwa ameachana na mpenzi wake aliyedumu naye kwa miaka minne lakini kinachomtesa akilini mwake ni fikra na mapenzi juu ya mpenzi wake huyo.

KIMSINGI IKO HIVI;
Kwa sababu ya mazoea na kushirikiana katika masuala au vitu vingi na mpenzi wako ndiyo maana huwa ni vigumu sana kumsahau lakini baada ya muda naamini unaweza kusahau. Kipindi cha maumivu ya mapenzi ni kama kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu ambapo kila mtu anatamani chama chake kishinde na kama kipindi hiki cha uchaguzi kikitumika vibaya na kusababisha uvunjifu wa amani, basi wananchi wa nchi husika watakuwa wamekosa busara kwani uchaguzi ni suala la mpito na ndivyo ilivyo kwa maumivu ya mapenzi, huwa ni suala la mpito tu.

Sababu za wanaume kuwa mapenzini na wafanyakazi wa ndani (house girls)



Miongoni mwa watu ambao wanatakiwa kupewa heshima zote hapa duniani ni wadada wa kazi za nyumbani ( house girl),  maana hawa wamekuwa wana msaada mkubwa sana katika familia zilizo nyingi. Wamekuwa wakiwasaidia wenye nyumba katika kutimiza majumu mbalimbali ambapo mimi binafsi naamini kazi hizo wanazozifanya na wafanyakazi hao  kama wenye nyumba wakipewa wazifanye ni lazima zitawashinda hii ni kutokana na ugumu na wingi wa kazi hizo.

Lengo la kuja hapa si kuwasifia wadada wa kazi ila nafanya hivyo kwa sababu najikuta naguswa sana na umuhimu wa wadada wa kazi katika kutekeleza majukumu mbalimbali wayafanyayo. Kama wewe ni mdada wa kazi na unasoma makala hii basi mwenyezi Mungu akautie nguvu kila wakati katika kutekeleza  yaliyo mema na yenye kumpendaza bosi wako.

Baada ya kusema hayo naomba sasa naomba nilonge na wakina mama wote walioko kwenye mahusiano ya  ndoa ambao wanaishi na wafanyakazi wa ndani.

Hivi uliwahi kujiuliza ni kwanini wanaume wengi hupenda kuwa na mahusiano na wasichana wa ndani? Kama hujawahi kujiuliza basi leo nitakupa ukweli usiojua kuhusu jambo hili.

Ipi hivi wanandoa wanapoingia katika mahusiano ya kimapenzi huwa kunakuwepo na upendo wa kweli baina yao mwanzoni kabisa mwa mahusiano hayo ila kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo upendo unavyozidi kushuka, jambo hili hutokea hii ni kwa sababu ya wanandoa hao hufika hatua wanazoeana sana hivyo kila mmoja wao kumuona mwenzake ni mtu wa kawaida sana hivyo kupelea kushuka kwa heshima baina yao.

Hivyo inapofika hatua ya kwamba wandoa hao wamezoea na heshima imeshuka hivyo ndoa hubadilika mwelekeo na kuwa chungu kama shubiri,  na inapofika hatua hii mwanaume huwa haoni thamani tena ya mkewe.

Na kwa kuwa falsafa ya mahusiano inatuambia ya kwamba mwanaume huwa haitaji upendo kutoka kwa mkewe  katika suala zima zima la mahusiano, bali mwanaume huhitaji heshima ya kutosha kutoka kwa mke wake, hivyo inapofika kipindi mwanaume huyo haoni tena thamani na upendo kutoka kwa mkewe hivyo anaamua kung`aza macho yake kwa mtu ambaye atampa heshima.

Na kwa kuwa wewe mkewe umebadilika kitabia haupo kama ulivyokuwa zamani hivyo mwanaume huyo anaamua kwenda kwa mfanyakazi wako wa ndani, kwa kuwa mwanaume anaona heshima nyingi kutoka kwa mfanyakazi wa ndani kuliko kwako.

Nini kifanyike ili kuzua tabia ya mwanaume kutoka kimapenzi na wafanyakazi wa ndani.

Mosi; ewe mwanamke  ili mwanaume wako  asiwe na tabia hii ya kuwapenda kimapenzi wafanyakazi wako wa ndani unatakiwa kuelewa ya kwamba kitu ambacho humpa mwanaume tabasamu mwanana la kimapenzi ni pamoja na kumuonesha mwanaume huyo heshima iliyo ya kweli na si vinginevyo.

Pia si kila jukumu anatakiwa kufanya mfanyakazi wako wa ndani mengine unatakiwa kufanya wewe mwenyewe, kila wakati kumbuka majukumu yako ni yapi na majukumu ya kumpa mfanyakazzi wako ni yapi pia.

Mbili; Mwanaume achana na tabia hii kwani haitakusaidia kwa chochote zaidi ya kujenga mahusiano yaliyo mabovu baina yako na mpenzi wako. Lakini pia Afisa Mipango nakushauri ya kuwa kila wakati ewe mwanaume unatakiwa kukumbuka kiapo chako cha ndoa.

Tatu; Ewe mfanyakazi wa ndani tafadhari sana achana mara moja na tabia hiyo ya kufanya unayajua sana mapenzi, kilichokupelekea hapo ni kufanya kazi na si mengineyo kwani kama utaendelea na tabia hiyo utaweka sumu kwenye familia hiyo.  Muombe Mungu akupe na nawe kipenzi wa moyo wako.

Mwisho naomba nikutakie siku njema na majumu mema, endelea kutembelea Muungwana blog kila wakati.

Na. Benson Chonya

Wanawake wengi hupenda wanaume wenye sifa hizi katika mahusiano ya kimapenzi




Katika safari yeyote ile ya mahusiano ya kimapenzi baina ya mwanamke na mwanaume yapo mambo mbalimbali yanapaswa kuzingatiwa ili kufanya mahusiano hayo yaweze kudumu, na miongoni mwa vitu vitakavyofanya mapenzi yadumu ni pamoja na kuwako kwa tabia ambazo zitakazowasaidia wapenzi hao waweze kuelewana.

Muungwana blog inakusogezea kwako tabia  zifuatazo ambazo wanawake wengi huzipendelea kutoka kwa wanaume zao ili waweze kudumu katika mahusiano ya kimapenzi :

Mwanamke humpenda mwanaume mwenye kujali na kuheshimu hisia za mwanamke.
Endapo utapata mwanaume mwenye kujali hisia zako za kimapenzi basi huyo ndiye mwanaume sahihi kwako, kwani hukuna kitu kizuri kama kuwa kwenye mahusiano na mtu anajali hisia zako na si kuziumiza.

Mwanaume mwenye akili za utafutaji wa maisha.
Katika ulimwengu wa mahusiano hakuna kitu kizuri kama kumpata mwanaume mwenye akili timamu za utafutaji na upambanaji wa maisha, hivyo kila wakati ewe mdada mwenye uchu wa ndoa kama utaka mwanaume sahihi kwako basi unatakiwa kuhakimisha unashughurika na mwanaume mwenye akili za utafutaji wa kimaisha na si vinginevyo.

Mwenye kujua mwanamke anataka nini haswa.
Unajua wapo wanaume ambao ni mahili sana wa kusema fulani nakupenda sana, ila ukweli ukiwachunguza watu hao huongozwa na tamaa tu, kwani wapo wanaume wachache sana ambao wanaojua kiundani kuwa mwanamke anataka nini haswa. Ngoja nikuibie siri ewe mwanaume unayesmoama makala haya, mwanamke anahitaji kuona unamjali ili awe na amani ya moyo.

Mwanaume ambaye anathamimi na kumjali msichana.
Jambo ambalo mwanamke anahitaji kutoka kwa mpenzi wake ni upendo na kujaliwa, mwanamke mwenye hisia thabiti anapenda kuona mwanaume wake anamjali na kumpenda kila wakati na hivyo kila wakati wanaume wanashuriwa kuwajali wapenzi wako kadri wawezavyo.

Mwanaume mwenye kukujulia hali kila wakati.
Asikwambie mtu mapenzi ya kweli ni uzao utokanao na mawasiliano thabiti baina ya wapenzi hao, hivyo mwanamke hupenda mawasilino mazuri kutoka kwa mume wake, hivyo ewe mwanaume kila wakati unatakiwa kumjali mwenza wako kwa kuongeza mawasiliano kwani hii ndiyo njia pekee ya kuonesha ujali hatiamaye muweze kusumu katika mahussssianao yenu.

Mwanaume mwenye kujali ndugu na jamaa na marafiki wako wa karibu.
Kila mwanamke anapenda kuona mbali na kuonesha upendo wako kwake pia napenda kuona unajali watu ambao wanamzunguka pia. Watu kama wazazi, ndugu na marafiki unatakiwa kuonesha upendo wako kwao pia hii itawafanya watu hao waone kuwa unafaa sana.

Asante kwa kusoma makala haya kutoka hapa Muungwana blog, tukutakie siku njema na utekelezaji mwema.

Na. Benson Chonya.

Zijue faida za kumsifia mkeo/mmeo au mpenzi wako



Kuna mengi mazuri ambayo huenda mpenzi wako aliwahi kukufanyia, je uliwahi kumshukuru kwa kukufanya ufarijike? Naamini Mungu amekujaalia kuwa na mpenzi mzuri, mwenye kila sifa ambayo ulitamani awe nayo, je ulishawahi kumsifia hata kwa kumwambia ni mzuri?

Huenda ulishawahi kufanya hivyo lakini kwa taarifa yako wapo ambao wanahisi kufanya hivyo eti ni ulimbukeni. Ulimbukeni? Kumsifia mpenzi wako  unaona ni ulimbukeni wakati wataalam wa masuala ya mapenzi wanaeleza kuwa, wanawake ni watu wanaopenda kusifiwa sana hata kwa madogo wanayoyafanya.

Unaona hatari gani kumsifia mpenzi wako kuwa ni mzuri? Unadhani unatumia nguvu gani kumsifia mpenzi wako kutokana na mahaba mazito anayokupatia?

Kwa taarifa yako unaweza kuona ni kitu kidogo sana  lakini madhara yake kwenye penzi ni makubwa.

Kumsifia mpenzi wako kwa yale anayokufanyia kuna faida nyingi sana lakini kwa leo nitagusia chache. Kwanza kunaongeza mapenzi. Mume/mke anaposifiwa kuwa anajua mapenzi hata kama si kwa kiwango kikubwa, anafarijika sana.

Unapomwambia mpenzi wako: ‘Dear nashukuru kwa mapenzi uliyonipa jana, umenipa furaha ya ajabu ambayo siamini kama kuna mtu mwingine wa kunipa, nakupenda sana’.

Maneno kama haya hutumii nguvu wala muda mwingi kuyafikisha kwa mpenzi wako lakini uzito wake ni mkubwa. Kwanza anajihisi aliyekamilika kwa kufikia hatua ya kufanya mambo yakamridhisha mpenzi wake na kwa mazingira hayo anaamini huwezi kumsaliti. Hisia hizo zitamfanya azidi kukupenda.

Hilo ni kwa wote yaani kwa mwanaume na mwanamke. Lakini pia unapomsifia mpenzi wako kwa yale anayokufanyia, unamfanya aongeze kasi ya kukufanyia ili nawe uzidi kumpenda.

Kwa mfano, unapokutana na mpenzi wako kisha ukamwambia ‘umependeza kweli mpenzi wangu, nazidi kukupenda kwa unavyovaa’.

Mtu anayeambiwa maneno haya atajitahidi sana siku zote aonekane nadhifu na wa kuvutia kwa mpenzi wake akijua kwamba, akivaa ilimradi kuvaa, hatamfurahisha mpenzi wake. Kwa maana hiyo kumsifia mpenzi wako kunamfanya azidi kuwa bora.

Lakini kusifia kusiwe kwa kinafiki. Usimsifie mpenzi wako eti ili kumfanya ajione bora kumbe katika uhalisia siyo hivyo.

Tusifiane pale inapobidi huku tukijua kuwa kwa kufanya hivyo tutapata faida. Tusiwe na tabia ya kuchukulia poa kila tunachofanyiwa na wapenzi wetu.

Kama kakuridhisha kimapenzi, msifie kwamba yeye ni muhimu kwako kwa kuwa amekupa ulichotarajia. Amekupikia chakula kizuri, msifie kuwa yeye ni mpishi mzuri. Hiyo italinogesha penzi na utashangaa kila siku inayokwenda kwa Mungu penzi lenu linachanua.

Lakini mbali na hayo, unatakiwa kuridhika kwa kile unachokipata kutoka kwa huyo mpenzi wako ulinaye kwa sasa. Najua kwenye uhusiano wengi tumetoka mbali. Wapo waliowahi kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja huko nyuma na kila mmoja alikuwa na kiwango chake cha kukuridhisha.

Inawezekana kuna ambaye unamkumbuka kwa mapenzi mazito aliyokuwa anakupa zaidi ya huyo uliyenaye. Hiyo ni historia, imepita! Kama huyo uliyenaye si mtaalam sana wa kukufikisha pale unapopataka, ridhika na hicho kidogo unachokipata endapo atakuwa anaonesha kukupenda kwa dhati.

Mpe moyo, msifiesifie kidogo kwa hiyo furaha kiduchu anayokupa huku ukiamini kuwa, atabadilika kadiri siku zinavyokwenda.

Kumbuka cha msingi katika maisha yetu ni kumpata mtu mwenye mapenzi ya kweli na si kumpata anayeweza kukuridhisha katika mambo kadha wa kadha.

Ishara zitazokuonyesha kama mwanaume uliyenaye anakupenda kweli



Siku zote ni lazima uelewe ya kwamba mwanaume kukwambia anakupenda tu hii haitoshi, bali yapo mambo ya msingi ambayo unatakiwa kuyoana kutoka kwa mwanaume huyo kama kweli anakupenda au anakudanganya tu.

Pia mara zote tunaambiwa wa watalamu wa masuala ya mahusiano kuwa upendo wa kweli huwa haujifichi bali huonekana kwa maneno na matendo pia.

Hivyo zifuatazo ndizo ishara zitakazokuonesha kama mwanaume uliyenaye anakupenda au aunakudanganya:

1. Mwanaume mwenye mapenzi ya dhati na wewe ni yule mwenye kukuonesha hisia zake za wazi za kimahusiano pasipo hata kukuonea aibu mpenziwe, hii ni kwa sababu kama nilivyosema hapo awali upendo wa kweli huwa haujifichi, hivyo kama kweli anakupenda kwa dhati zipo ishara za kihisia ambazo ni lazima uzione kutoka kwa mwanaume huyo.

Hisia za wazi ni kama vile matendo dhidi ya maneno ni lazima yaonekane waziwazi, hisia za wazi ni lazima mpenzi wako awe wazi kuwaeleza watu wengine kuhusu mahusiano yenu lakini pia hisia za wazi ni lazima mwanaume awe tayari kuongozana na wewe kila mahali pasipo kuona aibu yeyoto ile.

2. Mwanaume mwenye mapenzi ya dhati na wewe ni yule mwenye kukujali wewe kila wakati, hapa namaanisha ni lazima awe tayari kukusaidia katika shida na raha zote kila inapowezekana kuweza kukusaidia kufanya hivyo. Mapenzi ni hisia hivyo kila wakati ni lazima nafsi yako ione kuwa upo sehemu salama na haujutii kuwa mahala hapo.

3. Mwanaume mwenye mapenzi ya dhati na wewe ni yule mwenye kujali na kukukupa heshima zote unazostaili kuzipata kama mwanamke, hivyo kila wakati ni lazima atambue uwepo wako na kukupa uhuru pia wa kufanya mambo yako ya msingi na yakuleteayo mafanikio binafsi.

4. Mwanaume mwenye kutambua thamani ya mahusiano ni lazima atakuwa ni msikilizaji mzuri wa yale unayomwambia, hii ni kwa sababu wanaume wamejawa na misingi ya kibabe yaani yeye  anaamini yeye ndiyo kila kitu kitu hivyo haitaji ushauri wowote kutoka kwa mpenziwe. Mahusiano ya kweli hujengwa na pande zote mbili kuwa na mazungumzo na masikilizano yaliyo mwanana.

5. Mwanaume ambaye unamhitaji katika maisha yako ni yule ambaye hawezi kukuzuia kufanya kitu ambacho unakipenda kutoka moyoni mwako. Wanaweke wengi  wanakufa na uwezo mkubwa ulipo ndani yao hii ni kwa sababu ya wanaume walionao. Wengi huwazuia kufanya vile vitu wanavyofanya huku wakiamini ndio upendo wenyewe kitu ambacho si kweli hata chembe.

Hizo ni ishara za wazi ambazo zitakuonesha kama mwanaume uliyenaye anamapenzi ya kweli au anakupotezea muda tu. Endelea kutembelea Muungwana Blog.

Na. Benson Chonya

Zijue faida saba (7) za kuwa Single



Katika sayari hii ya dunia kuna baadhi ya watu wanakwambia mapenzi ndiyo yanayoiendesha dunia, hii ni kwa sababu asilimia kubwa ya watu wengi wametawaliwa na mawazo ya kimapenzi.

Pamoja na kuwapo kwa kundi hilo la watu wanaoamini hivyo lakini pia wapo baadhi ya watu  huamini ya kwamba mapenzi hayana  faida yeyote ile.

Kundi hili la watu hao hujikuta wakitoka kwenye mahusiano, na sababu zinazopelepekea wao waamini hivyo mara nyingi huwa zinatokana na maumivu ya kutendwa na mtu ambaye alikuwa anamuamini na leo hii hayupo na mtu huyo tena kwenye mahusiano.

Tuakiachana na hayo, karibu sana hapa Muungwana Blog kwani tumekusogezea faida za kuwa single katika ulimwengu huu.

1. Mtu anapokuwa single anakuwa na uhuru wa muda wa kufanya mambo yako binafsi pasipo kupelekeshwa na mtu yeyote yule. Uhuru huu wa muda ni ule wa kufanya mambo yake na ya kijamii pia.

2. Mtu ambaye yupo single unakuwa na uhuru pia wa kufanya kile inachokitaka/ anachokipenda. Unapokuwa kwenye mahusiano kunakosekana uhuru wa kufanya vitu uvipendavyo hii ni kwa sababu unaweza ukawa unapenda kufanya jambo fulani ila kwa kuwa upo kwenye mahusiano ya kimapenzi huyo mpenzi wako akakuzuia kufanya jambo hilo kwa kuwa jambo hilo halimpendezi.

3. Unapikuwa single unakuwa hauna hisia mpelekesho, hisia mpelekesho ni zile hisia za kimapenzi ambazo zinakufanya ifikiri sana kuhusu mambo yanayohusu mapenzi, kwa mfano hivi hujawahi ona mtu anakurupuka usiku wa manane anampigia simu mpenziwe? bila shaka umewahi kuona, hii ni tabia inayokwenda sambamba na kitu kinachoitwa wivu. Hivyo unapokuwa single unakuwa hauna wivu kwa sababu unakuwa hauna mtu ambaye anakufanya uwe hivyo.

4. Unapokuwa single hakuna lawama zinazohusu mahusiano ambazo zitakuwa zinakuhusu wewe. Unapokuwa kwenye mahusiano yapo malalamiko mengi ambayo yatakuwa upande wako, vitu kama kwanini hupokei simu yangu na mambo mengine kama hayo yatakuwa mbali na wewe.

5. Utaishi maisha marefu yenye mjumuiko wa amani ya moyo pamoja usiokuwa na bugudha wala makwaluzano ya aina yeyote ile.

6. Kila siku Utalala usingizi mzuri.

7 Faida nyingine ya kuwa single utaongeza mwenyewe.

Jinsi ya kutumia sekunde tatu kumtongoza mwanamke



Habari za muda huu mdau na mfuatiliaji wa makala mbalimbali zinazokujia kupitia mtandao huu wa Muungwana Blog bila shaka umzima wa afya na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku.

Naomba nichukue walau dakika zako chache kuweza kukujuza mbinu hii ya sekunde tatu kuweza kumtongoza mwanamke yule umtakaye na endapo utatumia sekendu hii tatu mwanamke huyo ni lazima atakuwa wako.

Sekunde tatu ni sekunde za maangamzi dhidi yako na yule unayemuona mbele yako. Endapo ukimwona mwanamke ambaye unataka kumtongoza, kwa kawaida kuna zile sekunde tatu za kwanza ambapo unafaa uchukue hatua kabla ile sauti ambayo inajaribu kuongea na wewe kukuzuia kufanya hivyo.

Tunasisitiza uchukue hatua ya kuweza kumtongoza mwanamke huyo ndani ya sekunde tatu kwani ukishindwa kufanya hivyo basi mwanamke huyo atapita bila ya wewe kuweza kufanya hivyo.

Kila mwanaume akichelewa kuapproach mwanamke kuna ile sauti ambayo inaanza kukuongelesha kwamba sijui hamna kitu hapo, hii ndiyo ile sauti ambayo inawafanya wanaume wengi wabaki kuwa single milele.

kwahiyo la kufanya hapa ukimwona mwanamke unayetaka kumuapproach basi fanya fasta. Una sekunde tatu za kuweza kufanikisha mpango mzima la sivyo kila msichana mzuri anayepita mbele ya macho yako utaendelea kumuita shemaji.

Endelea kutembelea Muungwana Blog kila wakati.

Na. Benson Chonya

Hivi Ndivyo Zari Alivyowaumbua Tanasha na Shilole

Mchumba wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch ameendelea kutengeneza vichwa vya habari Bongo, Amani linaye....